AZAM FC YAWACHAPA CHIPUKIZI 1-0 NA KUONGOZA KUNDI A MAPINDUZI


BAO pekee la mshambuliaji Msenegal, Alassane Diao dakika ya 12 limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Chipukizi United katika mchezo wa Kundi A Kombe la Mapinduzi usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.
Ushindi huo unaifanya Azam FC iongoze kundi hilo kwa pointi zake nne sasa ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Mlandege na Vital’O ya Burundi zenye pointi mbili kila moja, wakati Chipukizi United sasa inashika mkia kwa pointi yake moja.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post