LIVERPOOL YAREJEA KILELENI BAADA YA KUICHAPA BURNLEY 2-0 TURF MOOR


TIMU ya Liverpool imefanikiwa kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Burnley FC
leo Uwanja wa Turf Moor mjini Burnley.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Darwin Núñez dakika ya sita na Diogo Jota dakika ya 90 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 42 katika mchezo wa 19 na kupanda tena kileleni mwa Ligi Kuu wakiizidi Arsenal pointi mbili, ambayo pia ina mechi moja mkononi.
Kwa upande wao Burnley wanabaki na pointi zao 11 za mechi 19 sasa katika nafasi y 19 kwenye Ligi y timu 20, ambayo mwisho wa msimu tatu zitateremka hadi Ligi ya Championship.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post