MAN UNITED YASONGA MBELE KOMBE LA FA ENGLAND


TIMU ya Manchester United imefanikiwa kwenda Raundi ya Nne ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Wigan Athletic jana Uwanja wa DW mjini Wigan.
Mabao ya Manchester United yamefungwa na Diogo Dalot dakika ya 22 na Bruno Fernandes kwa penalti dakika ya 74 na kwa ushindi huo kikosi cha Kocha Mholanzi, Erik ten Hag kitakutana na mshindi kati ya Newport County na Eastleigh.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post