SIMBA SC YASAJILI BEKI WA TANZANIA PRISONS


KLABU ya Simba imemtambulisha beki Edwin Charles Balua (22) kuwa mchezaji wake mpya wa sita dirisha hili dogo kutoka Tanzania Prisons ya Mbeya.
Wengine ni viungo wawili, Msenegal Babacar Sarr (26) kutoka US Monastir ya Tunisia na winga, Ladaki Juma Chasambi (19) kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Wapo pia washambuliaji, Muivory Coast Freddy Michael Kouablan (25) kutoka Green Eagles ya Zambia ambako alikuwa anaongoza kufunga mabao kwenye Ligi Kuu ya nchi hiyo, Mgambia, Pa Omar Jobe (25) kutoka Zhenis ya Kazakhstani na Saleh Karabaka Kikuya (23) kutoka JKU ya Zanzíbar.
Katika dirisha hili dogo Simba SC pia imeachana na washambuliaji wake wawili wa kigeni, Mkongo Jean Othos Baleke na Mzambia, Moses Phiri, hivyo kufanya jumla ya wachezaji sita iliyowaondoa dirisha hili dogo.
Wengine ni wazawa viungo Jimson Stephen Mwanuke (24), Nassor Yahaya Kapama (27) na washambuliaji Shaaban Iddi Chilunda (25) na Mohamed Mussa Saleh (22).


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post