YANGA SC YAAJIRI MAAFISA WANNE WAPYA


KLABU ya Yanga imeajiri Maafisa wanne wapya katika Idara tofauti kuziba nafasi za walioondoka na kuongeza nguvu ya utendaji katika maeneo mengine.
Hao ni pamoja na Maafisa wawili wa Idara ya Wanachama na Mashabiki, Khamis Jecha na Jimmy Kindoki, Afisa Idara ya Habari na Mawasiliano, Willy Shemoka na Mkurugenzi wa Idara ya Masoko, Ibrahim Samuel.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post