TIMU ZA AFRIKA ZOTE ZATUPWA NJE KWENYE SOKA OLIMPIKI

TIMU zote za Afrika jana zimefungishwa virago kwenye michezo ya Olimpiki inayoendelea Jijini Tokyo, Japan.
Ivory Coast walitupwa nje na Hispania baada ya kuchapwa 5-2 Uwanja wa Miyagi mjini Rifu katika michezo hiyo inayohusisha vijana chini ya umri wa miaka 23 wakiongezewa watatu waliozidi umri huo.
Safari ya Misri ikahitmishwa na Brazil baada ya kuchapwa 1-0, bao pekee la Matheus Cunha dakika ya 37 Uwanja wa Saitama 2002.

Mechi nyingine za Robo Fainali, wenyeji Japan waliitoa New Zealand kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 0-0 Uwanja wa Kashima, wakati Mexico iliichapa Jamhuri ya Korea Republic 6-3 Uwanja wa Nissan Jijini Yokohama.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post