TIMU ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imefanikiwa kwenda Robó Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa penalti 8-7 dhidi ya Misri usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Laurent Pokou mjini San-Pedro nchini Ivory Coast.
DRC walitangulia kwa bao la mshambuliaji wa Young Boys ya Uswisi Meschack Elia Lina dakika ya 37, kabla ya mshambuliaji wa Nantes ya Ufaransa, Mostafa Mohamed kuisawazishia Misri kwa penalti dakika ya 45.
Pamoja na Misri kumaliza pungufu kufuatia mchezaji wake Hamdi Mohamed kutolewa kwa nyekundu katika dakika za nyongeza kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano, lakini ilifanikiwa kumaliza dakika 120 na kwenda kwenye mikwaju ya penalti.
Sasa DRC itakutana na Guinea ambayo mapema jana iliitoa Equatorial Guinea kwa kuichapa 1-0, bao pekee la mshambuliaji wa Le Havre ya Ufaransa, Mohamed Lamine Bayo dakika ya 90 Olympique Alassane Ouattara Jijini Abidjan.