TIMU ya Senegal imevuliwa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kufungwa kwa penalti 5-4 na wenyeji, Ivory Coast katika mchezo wa Hatua ya 16 Bora kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro mjini Yamoussoukro.
Mshambuliaji wa Al Shabab, Mouhamadou Habibou Diallo alianza kuifungia Senegal dakika ya nne tu akimalizia krosi ya mkongwe, Sadio Mané wa Al Nassr kabla ya Franck Kessié wa Al Ahli, zote za Saudà Arabia kuisawazishia Ivory Coast kwa penalti dakika ya 86.
Sasa Ivory Coast itakutana na Cape Verde katika Robi Fainali ambayo iliitoa Mauritania kwa kuichapa 1-0 katika mchezo uliotangulia jana, bao pekee la Ryan Mendes kwa penalti dakika ya 88 Uwanja wa Félix Houphouët-Boigny Jijini Abidjan.