SIMBA SC YAIRARUA TEMBO 4-0 NA KUSONGA MBELE ASFC


TIMU ya Simba SC imefanikiwa kwenda Raundi ya Tatu ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federatión Cup (ASFC) baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Tembo ya Tabora leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na viungo, Luis Miquissone wa Msumbiji dakika ya 11, Mrundi Saido Ntibanzokiza dakika ya 31 na washambuliaji wapya, Saleh Karabaka dakika ya 81 na Mgambia, Pa Omar Jobe dakika ya 83.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post