KMC BADO WAPO WAPO SANA LIGI KUU WAIPIGA MBEYA CITY 2-0 UHURU


TIMU ya KMC ya Kinondoni imefanikiwa kusalia Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbeya City jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya KMC katika mchezo huo wa marudiano wa mchujo wa kukwepa kuteremka daraja yamefungwa na Daruwesh Saliboko dakika ya tatu na Awesu Awesu dakika ya 28.
KMC inabaki Ligi Kuu kwa ushindi wa jumla wa 3-2 kufuatia kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Jumanne Jijini Mbeya na sasa Mbeya City itakwenda kumenyana na Mashujaa ya Kigoma kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post