DODOMA JIJI YAICHAPA KMC 1-0 AZAM COMPLEX


BAO pekee la Paul Peter dakika ya 71 limeipa Dodoma Jiji FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. 
Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji FC wanafikisha pointi 12 na kupanda nafasi ya nne, wakati KMC inayobaki na pointi zake 12 pia inashukia nafasi ya tano ikizidiwa wastani wa mabao na Walima Zabibu 
baada ya wote kucheza mechi nane.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post