JKT QUEENS YAPANGWA NA MAMELODI LIGI YA MABINGWA AFRIKA


TIMU ya JKT Queens imepangwa Kundi A katika Ligi ya Mabingwa Afrika Wanawake pamoja na wenyeji, Athletico FC d’Abidjan ya Ivory Coast, Sporting Casablanca ya Morocco na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Kundi B linaundwa na mabingwa watetezi, AS FAR ya Morocco, Ampem Darkoa ya Ghana, Huracanes FC ya Equatorial Guinea na AS Mande ya Mali.
Michuano hiyo itaanza Novemba 5 hadi 19 mechi zikichezwa viwanja vya Laurent Pokou Jijini San Pedro na Amadou Gon Coulibaly Jijini Korhogo.




Post a Comment (0)
Previous Post Next Post